Serikali yawapa Onyo kali wasimamizi wa viwanja Azam Complex na Nangwanda Sijaona, Mtwara



Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limewapa onyo kali wasimamizi wa viwanja vya Azam Complex, Dar es Salaam na Nangwanda sijaona, Mtwara kwa kukiuka Mwongozo wa Afya Michezoni katika mechi zao za kirafiki zilizofanyika tarehe 6 Juni, 2020 Jumamosi.

BMT imesema mechi hiyo iliyochezwa kwa kuhusisha timu ya mpira wa miguu ya Transit Camp na Namungo mtawalia, wasimamizi walishindwa kusimamia mashabiki katika sehemu ya viwanja hivyo kukaa umbali wa mita moja hivyo kukiuka taratibu za afya michezoni.


”Serikali kupitia BMT imewapa ONYO KALI wasimamizi wa viwanja vya Azam Complex, Dar es Salaam na Nangwanda sijaona, Mtwara kwa kukiuka Mwongozo wa Afya Michezoni katika mechi zao za kirafiki zilizofanyika tarehe 6 Juni, 2020 Jumamosi. Serikali imeeleza kuwa katika mechi hiyo iliyochezwa kwa kuhusisha timu ya mpira wa miguu ya Transit Camp na Namungo mtawalia, wasimamizi walishindwa kusimamia mashabiki katika sehemu ya viwanja hivyo kukaa umbali wa mita moja hivyo kukiuka taratibu za afya michezoni.”

”Serikali inaeleza kuwa hali kama hiyo ikijirudia tena viwanja vya Azam Complex, Dar es Salaam na Nangwanda Sijaona, Mtwara vitazuiwa kutumika kwa mechi za ligi zilizoruhusiwa bila onyo tena. Aidha Serikali imewataka wadau wote wakiwemo wasimamizi wa viwanja, timu mwenyeji ,viongozi wa michezo na afya na mashabiki wanakumbushwa kuchukua tahadhari kwani Serikali imerejesha michezo kwa nia njema wakati huu ugonjwa wa Covid-19 ukiwa umepungua sana lakini bado upo.”

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items