Ujerumani yaukosoa uamuzi wa Trump kuondoa wanajeshi wake

Afisa wa serikali ya Ujerumani anayeratibu uhusiano wa mataifa ya Ulaya na Marekani, Peter Beyer ameukosoa uamuzi wa Rais wa Marekani, Donald Trump wa kuwaondoa maelfu ya wanajeshi wake nchini Ujerumani.

Siku ya Ijumaa, afisa wa ngazi ya juu wa Marekani, alisema kuwa jeshi la Marekani litawaondoa askari wake 9,500 kutoka Ujerumani.

Beyer amesema uamuzi huo haukubaliki, kwa sababu hakuna afisa yeyote wa Marekani aliyeiarifu mapema Ujerumani, mshirika wake wa Jumuia ya Kujihami ya NATO. Beyer ameyatoa matamshi hayo wakati akizungumza na gazeti la Rheinische Post.

Kutokana na uamuzi huo wa Trump, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Heiko Maas amesema kwamba anasikitishwa na uamuzi huo, akiuelezea uhusiano kati ya Ujerumani na Marekani kuwa mgumu na usiotabirika.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items