Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya Walibya 16,000 wamepoteza makaazi yao kutokana na mashambulizi ya hivi karibuni kati ya vikosi vya serikali inayotambuliwa kimataifa na vikosi vya jenerali Khalifa Haftar.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya, UNSMIL umesema katika taarifa yake kwamba umeshtushwa na madhara yaliosababishwa kwa raia kutokana na mashambulizi yanayoendelea nchini Libya.
Ujumbe huo umesema mashambulizi ya hivi karibuni kwenye miji ya Tripoli na Tarhuna, yamesababisha zaidi ya Walibya 16,000 kukosa makaazi na kukumbana na mateso katika siku chache zilizopita.
Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umesema umefurahishwa na miito ya kuanza tena kwa mazungumzo ya kuumaliza mzozo wa Libya, siku moja baada ya Misri kutangaza mpango wa amani wa upande mmoja ambao unaungwa mkono na serikali ya upande wa mashariki.