Visa vya COVID-19 vyaongezeka Ujerumani

Idadi ya watu waliothibitika kuambukizwa virusi vya corona nchini Ujerumani imeongezeka kwa wagonjwa 214.

Kulingana na takwimu za Taasisi ya Robert Koch zilizotolewa leo, idadi ya maambukizi nchini Ujerumani imefikia hadi 184,193 na watu waliokufa ni 8,674, baada ya kuwepo vifo vingine 6.

New Zealand leo imetangaza kutokuwa na kisa chochote cha COVID-19, huku nchi hiyo ikiwa inajiandaa kuondoa vizuizi vilivyowekwa ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona.

 Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Andern amesema ingawa maambukizi ya virusi vya corona yamedhibitiwa, itahitajika kazi ya ziada kuifanya hali kubakia kuwa hivyo.

Wakati huo huo, wasafiri wanaongia nchini Uingereza kuanzia leo watatakiwa kujiweka katika karantini kwa muda wa wiki mbili.

Wale wote watakaoshindwa kutekeleza masharti hayo watatozwa faini. Urusi imetangaza vifo 112 ndani ya saa 24 na kuifanya idadi ya watu waliokufa kufikia 5,971.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items