Na Thabit Madai,Zanzibar.
Kutokana na Athari mbalimbali zilizosababishwa na maradhi ya Corona, Jamii visiwani husani Vijana wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuleta mabadiliko chanya pamoja na kuendeleza suala zima la Usafi wa mji wa huo ili kuzidi kuwavutia wageni kwenda kutalii pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa vijana hao.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa kampeni ya ‘Safisha Zanzibar’ Farida Nassor Mohamed wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Kamapeni hiyo inayotarijiwa kuzinduliwa siku ya Jumamosi katika Eneo la Forodhani Mjini Unguja.
Mkutano na Waandishi wa Habari ulifanyika katika ukumbi wa kituo cha kulea vijana pamoja Ushauri nasaha cha ZANLEGAL kilichopo Chukwani Unguja.
Kampeni ya Safisha Zanzibar ni kampeni iliyoandaliwa na wanaharakati vijana na kufadhiliwa na taasisi mbalimbali za maendeleo kama vile Ocean kind, zan lake, save the ocean pamoja na Zan legal.
Mratibu huyo Farida Nassor alisema kwamba vijana wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuleta mabadiliko katika jamii hususanikuendeleza usafi wa mji wa Zanzibar.
“Ukweli kuwa Zanzibar ni kituo na kitovu cha utalii hivyo tukiwa kama vijana tunapaswa kuendeleza zima la usafi wa mji wa Zanzibar ili kuongeza kivutia kwa wagenimbalimbali kuja kutembelea visiwa hivi”alisema Farida.
Akizungumzia kuhusu Kamapeni ya Safisha Zanzibar,Mratibu huyo alisema kampeni hiyo ina lengo la kuwahamasiasha vijana, watoto na jamii kwa ujumla umuhimu wa kusafisha mi uwe katika hali ya usafi.
“Kampeni hii inalengo la kuwahamasisha jamii nzima ya Zanzibar hususani vijana na watotowawe na mawazo ambayo si mgando katika kusafisha mji nakuwavutia watalii kuja kwa wingi”alisema Farid.
Aliongeza kusema kwamba ili Sekta ya utalii izidi kupanuka zaidi ni vyema jamii, Serikali na taasisi bimnafsi kuwaunga mkono katika harakatiza kusafisha mji uwe katika hali ya usafi.
“Watalii wanavutika kwenda katika maeneo ambayo yapo katika hali ya usafii hivyo ili kukuza sekta ya utalii jamii Serikali na sekta binafsi zinapaswa kuwa kuwa pamoja katika harakati za kuunga mkono kampeni hiyo”alisema Farida.
Farida alifahamisha kwamba Kampeni hiyo inatarijiwa kuanza katika meneomatatu, Forodhani, Nungwi na Jambiani huku zaidi ya watu 200 wakitarajiwa kushiriki.
Katika hatua nyingine Farida aliwaomba wananchi visiwani humo kujitokeza kwa wingi katika kampeni hiyoya Safisha Zanzibar ambapo watapata elimu kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na kusafisha.
“Sasa niwaombe wanachi hususani vijana, taasisi za vijana kuja kwa wingi siku ya Jumamosi forodhani kuanza kampeni hii ya Safisha Zanzibar ambapo kutatolewa elimu na tutaanza kusafisha baadhi ya maeneo ndani ya mji mkongwe wa Zanzibar”alisema farida.
Nae Asya Mwadini Mohamed kutoka katika taasisi ya ocean kind alisema kwamba taasisiyao imeamua kushiriki katika kampeni hiyo baada ya kuoana umuhimu wa kuelimisha jamii kusafisha Zanzibar.
“Sisi tumekuwa tunaprogram mbalimbali za kutunza mazingira hivyo lilivyokuja wazo hili tuliamua kuliunga mkono kwa asilimia zote ili kuweka mji wa Zanzibar katika hali ya usafikabisa”alisema Asya.
Kmapeni ya Safisha Zanzibar inatarajiwa kuzinduliwa Juma mosi katika eneola Forodhani majira ya saa mbili na nusu Asubuhi na kuuhudhuriwa na taasisi mbalimbaliza Serikali na binafsi.
