Kufuatia kifo cha George Floyd, Wajumbe wa chama cha Democratic katika Baraza la Wawakilishi wamewasilisha mswada wa sheria za kuimarisha udhibiti wa polisi.
Miongoni mwa mambo wanayopendekeza ni kupigwa marufuku mshukiwa kugandamizwa shingo, kurahisisha malalamiko dhidi ya polisi na kuwezesha uchunguzi huru.
Mswada huo haujatoa wito wowote wa kupunguza au kuondoa ufadhili wa polisi. Nafasi za kupitishwa mswada huo hazijulikani.
Wademocrat wanalidhibiti baraza la wawakilishi, lakini Baraza la Seneti linatawaliwa na Warepublican wa Rais Donald Trump.
