Wafanyakazi 1,593 wafukuzwa kazi "Scandinavian Airlines"

Shirka la ndege la Scandinavian Airlines (SAS) limewafukuza kazi wafanyakazi 1593 nchini Denmark.

Hii ni kutokana na hali mbaya ya kiuchumi iliyosababishwa na mlipuko wa virusi vya Corona ulimwenguni kote.

Meneja wa Vyombo vya Habari na Mahusiano ya Umma wa SAS nchini Denmark, Sille Beck-Hansen, amesema kampuni hiyo imewafukuza jumla ya  marubani 176, wafanyakazi wa "Cabin Crew" 684, maafisa wa utunzaji wa ardhi 586, wafanyikazi wa kiufundi 96 na watendaji 51 na kupelekea idadi ya jumla ya wafanyakazi waliofukuzwa kazi kufikia 1593.

Kulingana na Beck-Hansen, janga la Covid-19 limeathiri kwa kiasi kikubwa Shirika hilo la Ndege la "Scandiavia Airlines"..

Akisisitiza kwamba kampuni hiyo, ambayo imepita katika kipindi kigumu, imebidi ichukue hatua hiyo kutokana na hali ngumu ya kiuchumi, Beck-Hansen amesema kuwa utaratibu wa ujenzi wa SAS huko Norway na Sweden haujamalizika bado.