Aliniteua kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, bila hiyana- Kikwete

“Wilaya hii ya Masasi ilikuwa na tatizo la njaa wakati ule, nikiwa Katibu CCM Masasi na DC tukabuni mradi wa kilimo cha muhogo hakikupendeza sana kwasababu Wamakuwa hawapendi sana kula ugali wa mihogo kama Mashemeji zangu Wamakonde, ila Mzee Mkapa alisimama nasi”-MSTAAFU KIKWETE\

“Wakati tunaanza mchakato wa Urais mwaka 1995 nilimueleza kuwa wewe ndiye unafaa kuwa Rais, ila baadaye nikasukumwa naamimi kugombea akanishinda, ila aliposhinda ingawa kura zetu zilikaribiana akaniteua kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, bila hiyana” -MSTAAFU KIKWETE