Barcelona wanasema VAR inaibeba Real Madrid


Rais wa klabu ya Barcelona,Joseph Maria Bartomeu amesema VAR inaipendelea Real Madrid tangu La liga iliporejea baada ya COVIC-19.

Rais wa klabu ya Barcelona,Josp Maria Bartomeu ameiponda teknolojia ya usaidizi ya waamuzi ambayo anadai imekua ikiipendelea Real Madrid tangu ligi iliporejea baada ya mapumziko ya dharula kufuatia janga la COVID-19.

Kauli ya Bartomeu inafuatia ushindi wa Real Madrid  wa bao 1-0 dhidi ya Athletic Bilbao,lililofungwa kwa mkwaju wa penati na Sergio Ramos na kuipa uongozi Los Blancos wa alama nne kileleni dhidi ya Barcelona na sasa wanakaribia kutwaa ubingwa wa La liga iwapo watashinda mechi tatu kati ya nne zilizosalia.

Katika mechi dhidi ya Athletic Bilbao,mwamuzi Jose Gonzalez aliamuru pigo la penati baada ya kutafsiri kupitia VAR kwamba nyota wa Bilbao Dani Garcia alimchezea rafu mlinzi wa Real Madrid Marcelo.

Kwa mujibu wa Bartomeu,anasema VAR imekua ikiinufaisha zaidi Real Madrid tangu kurejea kwa La liga  kwa kuwa hata katika mechi zao tano zilizopita ikiwemo dhidi ya Real Sociadad ambayo walishinda,kulikua na maamuzi yaliyowapa kipaumbele likiwemo la Karimu Bemzema kufunga bao ambalo kuna kiashiria cha kuushika na mkono mpira kabla ya kufunga bao ambalo liliwapa ushindi wa bao 2-1.