Na Faruku Ngonyani, Mtwara
Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara imetengewa kiasi cha fedha shilingi Bilioni moja kwa mwaka huu wa fedha 2020/2021 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa ofisi ya Halmshauri hiyo iliyopo makao makuu kata ya Mkunwa Mkoani Mtwara.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi Erica Yegella ambapo amesema kuwa kwa sasa Halmashsuri hiyo inatumia ofisi ya kata ya Mkunwa hvyo ni vyema sas kuanza maandalizi ya ujenzi wa ofisi zao.
Ikumbukwe ofisi za Halmshauri ya Wilaya ya Mtwara awali zilikuwepo ndani ya eneo la Halmashauri ya Manispaa Mtwara Mikindani kabla ya Serikali kuziamlisha ofisi za Halmashauri zote nchini zilizopo kwenye eneo la utawala wa Halmashauri nyingine kuhama na kuhamia kwenye maeneo yao.
Aidha Mkurugunzi huyo ameongeza kuwa kwa sasa Halmashauri hiyo wanasimamia kilimo cha umwagiliaji kinacholimwa katika vijiji vya Lilido na Chem Chem huku Serikali ikitoa fedha Zidi ya Milioni Mia saba kwa awamu tatu ili kuimarisha kilimo hiko.
Kwa Mwaka 2010 Serikali ilitoa fedha shilingi Milioni Mia Mia Tisa Sabini na moja huku kwa mwaka 2011-2012 zilitolewa Milioni Mia Tatu ,Mwaka 2012-2013 zilitolewa Milioni Mia Tatu Hamsni na kwa mwaka 2013-2014 zilitolewa Milioni Mia Mbili Ishirini na Moja.
Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara yenye Makoa Makuu yake Kata ya Mkunwa ina jumla ya Kata 21 na ndio Halmshauri kubwa kati ya Tisa zilizopo Mkaoni Mtwara.
