Kimbunga Hanna kimeipiga pwani ya mji wa Texas nchini Marekani na kusababisha maafa ikiwemo uharibifu wa mfumo wa kusambaza umeme na kuzusha kitisho cha kutokea mvua kubwa kwenye eneo hilo.
Licha ya kupungua nguvu, kimbunga Hanna kiliwasili na upepo mkali kwenye kisiwa cha Padre na kisha baadae kuipiga kaunti ya Kenedy mjini Texas kabla ya kusambaa kwenye jimbo hilo lmbayo tayari limeathiriwa kwa sehemu kubwa na janga la virusi vya corona.
Katika kitongoji cha Port Mansfield, upepo mkali uliosababsihwa na kimbunga hicho uliangusha miti na kuharibu mashamba ya miwa huku paa za nyumba kadhaa pia zilingolewa.
Gavana wa jimbo la Texas Greg Abbott amesema idara ya maafa ya serikali kuu imetangaza kimbunga hicho kuwa dharura ya taifa na itatoa fedha za kusaidia uokozi pamoja na juhudi za kurekebisha maeneo ya makaazi.
