Loading...

7/01/2020

Jacqueline Mengi afunguka kuhusu kuolewa tena


Mwanadada Jacqueline Ntuyabaliwe ambaye ni mjane wa Reginald Mengi, Jumatatu hii amejibu maswali ya mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliwapa fursa ya kuuliza chochote na wengi wakatiriria.

Katika sehemu hiyo ya maswali na majibu, vitu ambavyo huenda vikawashangaza wengi ni namna alivyoweka wazi umri wake kitu ambacho wadada wengi hupenda kutosema miaka yao.

Kwenye moja ya swali aliloulizwa na shabiki yake nikuhusiana na umri wake kwa sasa, Jacqueline bila kificho alimjibu SHABIKI huyo kuwa, “Nina miaka 41 ila najihisi kama nina miaka 21.” aliandika.

Pia mrembo huyo ambaye ni mama wa watoto wawili mapacha hakusita kuongelea masuala ya ndoa ambapo shabiki mmoja alimuuliza, “Utaolewa tena?” naye akajibu, “Sijui, ngoja tuone Mungu amenipangia nini.”

Mbali na hayo, shabiki mmoja alimuuliza kama anaweza kuingia kwenye Siasa siku moja, Jack hakusita kujibu swali hilo akiweka wazi kuwa, havutiwi kabisa na masuala ya Siasa, “Hapana, sina interest nayo kabisa” aliandika.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger