Kansela Merkel ausihi Umoja wa Ulaya kuwa na sauti moja dhidi ya China

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, ameelezea wasiwasi wake kuhusu sheria mpya ya usalama iliyotangazwa na China huko Hong Kong.

Merkel amesema Umoja wa Ulaya lazima uzungumze kwa kauli moja na China, ukiwa unataka kufanikisha mikataba yenye maslahi na umoja huo.

"Kwa msingi wa mazungumzo ya wazi pia tunazungumza juu ya utawala wa sheria na haki za binadamu na vile vile mustakabali wa Hong Kong ambapo tuna wasiwasi kuwa kanuni muhimu ya nchi moja, mifumo miwili inaharibiwa," amesema Merkel.

Merkel ameliambia baraza la wawakilishi wa majimbo kwamba kwa ushirikiano wa pamoja, nchi wanachama 27 wa Umoja wa Ulaya zina uwezo wa kutosha wa kufikia mikataba kabambe na China.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items