Pelosi: Urusi iwekewe vikwazo na Marekani

Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi ametoa wito kwa Marekani kuiwekea vikwazo idara ya ujasusi ya Urusi kwa kuwalipa wanamgambo wa Taliban kuwauwa wanajeshi wa Marekani huko nchini Afghanistan.

Mwanasiasa huyo wa chama cha Democratic pia amesema, ulu ya White House imepinga kuiwekea vikwazo idara ya ujasusi na sekta nyinginezo za ulinzi katika sheria za zamani zilizokuwa na lengo la kuiadhibu Urusi.

Pelosi pia alisema Urusi inapaswa kuwajibishwa kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani.

Rais wa Marekani, Donald Trump ambaye amekuwa akijaribu kujenga uhusiano mzuri na Urusi, amekana kuarifiwa juu ya suala hilo kabla ya kuripotiwa katika vyombo vya habari wiki iliyopita.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items