Kauli ya Mbwana Samatta baada ya Aston Villa kusalia EPL

Mshambuliaji wa Kitanzania na anayekipiga Ligi Kuu nchini Uingereza (EPL), Mbwana Samatta, amemshukuru Mwenyenzi Mungu pamoja na mashabiki mara baada ya timu yake ya Aston Villa kusalia katika Ligi hiyo.

Aston Villa imemaliza Ligi ikiwa katika nafasi ya 17 na matokezo ya mchezo wa jana ya sare ya 1-1 dhidi ya West Ham ndio yaliyoamua hatima yao ya kusalia katika Ligi au kushuka daraja.

“Narudisha shukrani kwa Mungu kwa kuamua niendelee kubaki kwenye ligi kuu ya England tena mwakani. Asanteni kwa wote mlioiombea kheri villa ili muendelee kuniona tena ktk ligi hii pendwa,” ameandika Samatta kwenye ukurasa wake rasmi wa #Instagram.

Itakumbukwa, samata aliunga na Aston Villa kuelekea mwishoni mwa msimu huo akitokea KRC Genk ya Ubelgiji ambapo alikuwa kinara wa upachikaji mabao katika klabu hiyo.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items