Meek Mill amwagana na mpenzi wake Milano


Penzi la Rapa Meek Mill na Mrembo Milan Rouge Harris, ama Milano limefikia mwisho, wameripotiwa kuachana.

Itakumbukwa, wawili hao walipata mtoto hivi karibuni. Meek Kupitia ukurasa wake wa #Twitter alitoa taarifa ya kuachana na Milano kwa kuandika, wameachana kwa uzuri tu na wamebaki kuwa marafiki na walezi wa mtoto wao.

Kwa mujibu wa Us Weekly, wawili hao waliamua kuachana kimya kimya wiki chache zilizopita.

Aidha, Sababu za kuachana kwao hazijaweka wazi huku kila mmoja bado anamfollow mwenzake kwenye kurasa zao za #Instagram.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items