Makamu wa Rais wa Gambia, Isatou Touray amekutwa na maambukizi ya COVID19 na kutokana na hilo, Rais Adama Barrow atajitenga kwa muda wa siku 14
Taarifa iliyotolewa na Serikali haikuelezea kwa undani kuhusu hali ya kiafya ya Touray (65) ambaye alitangazwa kuwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo mwaka jana
Gambia imerekodi jumla ya visa 326 na vifo 9 vya Corona Virus, idadi ambayo ni ndogo zaidi kuripotiwa kwa ukanda wa Afrika Magharibi
