Mamia ya Wafilipino wameandamana katika Mji Mkuu Manila leo wakipinga sheria mpya ya kupambana na ugaidi na masuala mengine.
Maandamano haya yamefanyika licha ya kitisho cha polisi cha kuwakamata waandamanaji kuelekea hotuba ya kila mwaka kwa taifa ya Rais Rodrigo Duterte.
Katika mji wa Quezon Kamanda wa polisi Debold Sinas amesema waandamanaji 4 waliokuwa kwenye gari la abiria wamekamatwa ila mamia wamekusanyika katika chuo Kikuu cha Ufilipino.
Makundi mengine ya waandamanaji wameandamana kwa kuchapisha video mitandaoni ikiwemo video moja inayotishia kuichoma sanamu ya Rais Duterte.
Uongozi umepiga marufuku mikusanyiko ya zaidi ya watu kumi ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona. Waandamanaji lakini wanasema serikali inatumia janga hilo ili kuzuia ukosoaji mkubwa katika masuala kadhaa ikiwemo jinsi ilivyolishughulikia janga hilo la virusi vya corona.
