Manaibu Waziri wawili watembelea mradi wa umeme wa JNHPP


Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akiwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya wametembelea mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) Rufiji na kuelezea kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo.

Aidha wamewataka Watanzania kuwa na Imani na mradi huo huku wakisisitiza makandarasi kufuata sheria na haki za ajira katika utekelezaji wa mradi huo.

Wakiongea katika eneo la mradi wa ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme wa Mwl, Julius Nyerere Manaibu Waziri hao licha ya kuridhishwa na maendeleo ya mradi pia wamewataka wanawake kushiriki kikamilifu katika mradi na kuacha kujiweka nyuma wakiamini kazi zile ziko nje ya uwezo wao huku wakisitiza kuwa umeme utakaozalishwa utakuwa mkombozi kwa wawekezaji wa viwanda na watanzania wote.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items