Mgombea ubunge jimbo la Tanga mjini ataka kura zake apewe Ummy Mwalimu


Katika hali ya kushangaza mmoja wa wanaoomba kuteuliwa na CCM kugombea ubunge Jimbo la Tanga Mjini, Chawambula Abdulnab amesimama wakati wa kujinadi na kumuombea kura mgombea mwenzake, Ummy Mwalimu na yeye kujitoa.