Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi,amerasimisha sheria inayowazuia maafisa wa zamani kugombea nafasi ya urais au ubunge bila kupata ruhusa kutoka baraza kuu la jeshi.
Vilevile nchi hiyo imezuia muunganiko wa vyama vya kisiasa.
Wakosoaji wanasema, sheria hiyo inampa mamlaka rais Sisi kuzuia mwanajeshi yeyote kupambana na yeye.
Mwaka 2018, mkuu wa jeshi wa zamani, Sami Anan, alikamatwa baada ya jeshi kumshutumu kuwa alikuwa anakata kuwania nafasi ya urais bila kupata ruhusa.
Jeshi la Misri limeonekana kuwa na nia ya kupata uongozi, viongozi wote wawili wa nchi hiyo wana historia ya kutoka jeshini tangu taifa hilo liwe Jamuhuri.
Sheria mpya sasa pia itaangalia washauri ambao wanapelekwa kwa magava.
