Kama ilivyotokea Ujerumani, Ufaransa, na Uhispania, Italia nayo sasa imetangaza kushuka kwa uchumi wake kwa sababu ya janga la virusi vya corona, kulingana na ofisi zao za takwimu.
Ufaransa ilirekodi kuporomoka kwa asilimia 13.8 ya uchumi katika robo ya pili ya mwaka. Huko nchini Uhispania, thamani jumla ya bidhaa zinazozalishwa imepungua kwa asilimia 18.5 - ambacho ni kiwango kikubwa mno katika historia ya nchi hiyo.
Italia pia inapambana na uchumi uliosinyaa kwa asilimia 12.4. Na, Jana, Ujerumani ilitangaza kushuka kwa karibu asilimia 10 ya uchumi wake, na Marekani imeshuhudia kuanguka kwa uchumi wake kwa thuluthi moja.