Dk. Shein autaka uongozi na watendaji wa Wizara ya Vijana kuwajibika katika utekelezaji wa majukumu yao

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameutaka Uongozi na watendaji wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo  kuongeza kasi katika kipindi hiki kifupi kilichobaki kuelekea uchaguzi mkuu kwa kuwajibika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.


Dk. Shein amesema hayo Ikulu mjini Zanzibar, alipokutana na Uongozi  wa Wizara Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakati ilipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango kazi wa mwaka 2019/2020 na mpango kazi wa mwaka 2020/2021.


Alisema kuna umuhimu mkubwa kwa viongozi hao kuongeza kasi katika usimamizi na uwajibikaji wa majukumu ya kazi kwa kuzingatia kuwa  shughuli za Serikali zinapaswa kuendelezwa kama kawaida hadi pale awamu ijayo ya uongozi wa Serikali itakapochukua nafasi yake. 


Aliwataka watendaji hao kuendeleza mashirikiano yaliopo na  kubainisha kuwa hatua hiyo italeta tija kubwa.


Aidha, Dk. Shein alisema Zanzibar inahitaji kuwa na uwanja mkubwa wa kisasa utakaowezesha kufanyika shughuli mbali mbali za Kitaifa.


Alisema kuna umuhimu wa kuwa na uwanja wa aina hiyo,utakaokuwa na uwezo wa kufanyika matukio mbali mbali ya kitaifa, kama vile gwaride pamoja na michezo ya aina tofauti, ikiwemo mpira wa miguu.


Alisema uwanja uliopo wa Amani hauwezi kukidhi mahitaji ya wakati na hivyo akautaka uongozi wa Wizara hiyo kuangalia maeneo ya nje ya mji, 


Post a Comment

0 Comments