Kiongozi wa upinzani wa Belarus akimbilia nchini Lithuania kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi

Kiongozi wa upinzani wa Belarus Svetlana Tikhanouskaya ametorokea nchini Lithuania.Hii ni baada ya siku mbili za ghasia nchini Balarus kufuatia uchaguzi mkuu uliozua utata uliomrudisha tena mamlakani Rais Alexander Lukashenko.

Tikhanouskaya mwenye umri wa miaka 37 aliibuka kuwa mpinzani mkuu wa Rais Lukashenko, akiwania uongozi baada ya mume wake kufungwa jela.

Kumekuwa na hali ya wasiwasi juu ya aliko kiongozi huyo baada ya timu yake ya kampeni kusema jana Jumatatu kuwa hawakumpata kwa njia ya simu saa chache tu baada ya kufanya mkutano na maafisa wa tume ya uchaguzi nchini humo.

Mtu mmoja amefariki wakati polisi walipokabiliana na waandamanaji jana Jumatatu baada ya upinzani kumshutumu Lukashenko kwa kuchakachua matokeo ya uchaguzi huku kukiwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa viongozi wa Magharibi juu ya uchaguzi huo.

Post a Comment

0 Comments