Aug 2, 2020

Mafuriko nchini Afghanistan

Watu 16 wamepoteza maisha katika mafuriko kwenye mkoa wa Nangarhar mashariki mwa Afghanistan.

Ataullah Hogyani, Mnenaji wa Gavana wa Nangarhar amesema kuwa mvua kubwa imenyesha na kusababisha mafuriko katika eneo la Kuzkunar mkoa wa Nangarhar.

Ripoti imeonyesha kuwa watoto 15 ni kati ya wale waliopoteza maisha huku watu wengine wanne wakiwa wamejeruhiwa katika mafuriko hayo.

Hogyani amebaini kuwa nyumba nyingi pia zimeharibiwa kutokana na mafuriko.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger