Aug 2, 2020

Pombe yazidi kusababisha vifo India

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na unywaji wa pombe isiyokuwa halali imeongezeka na kufikia watu 86 katika jimbo la Punjab nchini India.

Kulingana na Press Trust of India, Waziri Mkuu wa Jimbo Amarinder Singh amesema angalau watu 86 ambao wamekunywa pombe isio halali wamepoteza maisha  katika mkoa wa Amritsar, Gurdaspur na Tarn Taran katika siku 4 zilizopita.

Wakati wa uchunguzi wa tukio hilo, Singh ametangaza kuwa maafisa 7, pamoja na polisi, wamesimamishwa kazi.

Akielezea tukio hilo kuwa la aibu, Singh amebaini kuwa vikwazo vikubwa vitawekwa kwa wale ambao watahatarisha afya ya umma.

Watu 25 walikamatwa katika operesheni zaidi ya 100 zilizozinduliwa kugundua na kufunga vituo vya utengenezaji wa pombe haramu katika jimbo lote

KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger