Matokeo ya Urais Belarus yapingwa

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula Von Der Leyen, ameitaka Belarus kuchapisha matokeo sahihi ya uchaguzi wa Rais, baada ya Rais Alexander Lukashenko kuibuka na ushindi mnono.

Nae Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Heiko Maas amesema kuna uwezekano vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Taifa hilo vikarejeshwa.

Rais Lukashenko ameshinda uchaguzi wa Rais kwa asilimia 80 ya kura na kupongezwa na jirani yake, Rais wa Urusi Vladmir Putin, lakini mataifa kadhaa ya Magharibi yameonyesha wasiwasi juu ya ushindi wake.

Watu kadhaa wamejeruhiwa na maelfu kukamatwa katika maandamano ya kupinga matokeo hayo nchini humo.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi