Mkuu wa mamlaka ya forodha Lebanon akamatwa kutokana na mlipuko


Mkuu wa mamlaka ya forodha ya Lebanon alikamatwa rasmi jana, baada ya kuhojiwa juu ya mlipuko mkubwa mjini Beirut mapema mwezi huu. 

Uchunguzi dhidi ya maafisa wanaokamatwa, unalenga kufahamu kwanini tani 3,000 za kemikali ya amoniamu nitrate zilikuwa zimehifadhiwa kwenye bandari. 

Shehena ya kemikali hiyo ndio ilisababisha mlipuko uliowaua watu zaidi ya 170 na kujeruhi wengine 6,000. 

Watu 30 bado hawajapatikana baada ya mlipuko wa Agosti 4 uliosababisha uharibifu wa karibu dola bilioni 15. Zaidi ya watu 70,000 wanaaminika kukosa ajira kutokana na mkasa huo. 

Rais wa Lebanon Michel Aoun amesema uchunguzi juu ya janga hilo ni mgumu na hautokamilika haraka. 

Naye msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric ameongeza kuwa watu wapatao 220,000 wanakadiriwa kupoteza kazi zao kutokana na mgogoro wa kifedha ulioanza Oktoba mwaka uliopita.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi