WAKATI Tanzania wakiungana na mataifa mengine Duniani kuadhimisha Siku ya vijana, Mkuu wa wilaya ya kaskazin B Rajab Ali Rajab amewataka vijana kudumisha suala la amani na utulivu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi wa oktoba
Amesema ili taifa liweze kufikia malengo katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo suala la kudumisha amani ni suala la muhimu katika nyanja zote
Akizungumza katika kongamano la vijana kuelekea kwenye maadhimisho ya siku ya vijana duniani mkuu huyo wa wilaya amesema kila mtu ana haki ya kushabikia chama chochote cha siasa lakini ana jukumu kubwa la kudumisha amani na utulivu nchi
Amefahamisha kuwa ofisi yake ipo wazi kupokea taarifa yoyote inayoashiria kujitokeza kwa vitendo vya uvunjifu wa amani hivyo ni vyema kwa mabaraza ya vijana shehiya kuwatoa taarifa za vitendo hivyo
Hata hivyo amewataka vijana kutumia fursa ya kuanzishwa mabaraza ya vijana ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali ikiwemo elimu ya ujasiriamali
Akizungumzia tatizo la vitendo vya udhalilishaji amewataka vijana kushirikiana ili kupinga vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikirkatisha ndoto za vijana wengi kushindwa kufikia malengo yao
Aidha ameyataka mabaraza ya vijana ya shehiya kuandaa mpango kazi ili kupata shughuli ya kujiendesha badala ya kutegemea serikali pamoja na wafadhili
Amefahamisha kuwa serikali kupitia raisi dokta Ali Muhammed shein imeamua kuanzisha mabaraza hayo ili kusaidia vijana kupaza sauti zao pamoja na kujadili matatizo yanayowakuta na kuyatafutia ufumbuzi
sambamba na hayo mkuu huyo wa wilaya amewapongeza vijana wote waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwani imeonesha wazi kuwa vijana wanavyojishughulisha katika sekta tofauti
Kwa upande wao baadhi ya vijana wameelezea mafanikio waliyoyapata katika mabaraza hayo kwani wameweza kuanzisha miradi mbalimbali pamoja na kuiomba serikali kuwa karibu na watu wenye ulemavu ili na wao waweze kunufaika na fursa mbalimbali
Amesema mafanikio mengi wameyapata ikiwemo kujuana na watu mbalimbali lakini pia wameweza kuanzisha Miradi ikiwemo kilimo cha miwa pamoja na njugu miradi ambayo imeweza kuwaingizia kipato na kugawana
Hata hivyo amewataka vijana kujiunga katika mabaraza hayo ili waweze kuunganisha nguvu katika kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya vijana kwa wakati
Amesem licha ya jitihada mbalimbali anazozichukua lakini bado kuna uelewa mdogo kwa vijana hasa walemavu ambao kuhusu kujiunga katika mabaraza hayo