Na Hamisi Nasri, Masasi.
WAKATI dirisha la uchukuaji fomu za ubunge za Tume ya taifa ya Uchaguzi( NEC) likifunguliwa Agosti 12 hii leo Mgombea Ubunge wa jimbo la Masasi mjinj kupitia Chama Cha demokrasia na Maendeleo( Chadema) Mustafa Swalehe amekuwa wa kwanza kufika katika ofisi ya msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Masasi mjini na kuchukua fomu rasmi ya kugombea nafasi hiyo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi fomu hiyo na msimamizi wa jimbo hilo ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ys mji Masasi, Gimbana Ntavyo,Swalehe alisema kuwa ameridhishwa na zoezi zima la uchukuaji wa fomu katika ofisi hiyo ya msimamizi na hakuna jambo lolote lile ambalo limekaa vibaya katika uchukuaji fomu hizo.
Alisema kabla ya kukakabidhiwa fomu hizo alipewa kwanza kwa ajili ya kuzisoma na kujiridhisha kama ziko sahihi na zimekamilika fomu zote zinazotakiwa kujazwa na wagombea wa jimbo hilo.
Swalehe alisema atakwenda kuzijaza fomu hizo kwa usahihi na kuzirejesha kwa wakati katika ofisi hizo za Tume ya uchaguzi jimbo la Masasi mjini.
Alisema Chama Cha demokrasia na Maendeleo( Chadema) kina matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi ndani ya jimbo hilo la Masasi.
Alisema kipaumbele chake cha kwanza katika kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa ubunge wa jimbo hilo ni kuhakikisha anatokomeza unjinga, maradhi na umasikini unaowakabili wananchi wa jimbo hilo.
"Wananchi wa jimbo la Masasi wamekuwa na ugumu wa maisha yao hivyo iwapo mkiniteuwa kuwa mbunge wa jimbo la Masasi kupitia Chadema nitaibadilisha Masasi," alisema Swalehe.
Naye mgombea ubunge wa jimbo hilo hilo la Masasi mjini kwa Chama wananchi( CUF) Hamza Machuma naye alikuwa mgombea wa pili kufika ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi jimbo hilo la Masasi na kuchukua fomu.
Machuma akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo alisema anaipongeza Tume ya uchaguzi kwa kuweka utaratibu mzuri katika kuchuchukua fomu za ubunge.
Alisema Cuf watahakikisha wanafanya kampeni za amani na utulivu na kwamba wataibuka ushindi kwa vile malengo yao ni kuwakomboa wananchi wa jimbo hilo katika Lindi la umasikini walionao.
Kwa upande wake Msimamizi wa Uchaguzi jimbo hilo la Masasi, Gimbana Ntavyo alisema atahikikisha ofisi yake inatenda haki kwa vyma vyote vya siasa
Alisema hakuna chama chotechote ambacho kitapendelewa hivyo kila chama kifuate taratibu zote zilizowekwa na Tume ya taifa ya uchaguzi(NEC) ikiwemo kusoma sheria ya uchaguzi na kanuni zake.
Vyama hivyo vyote vya Chadema na CUF hii leo walifika katika ofisi hizo za msimamizi wa uchaguzi jimbo la Masasi wakiwa na wakereketwa wao na wanachama, huku wakiwa na vyombo vya usafiri kama vile pikipiki za matairi matatu( guta) na bodaboda.
