Watu 81 wauawa katika zoezi la kukabidhi silaha Sudan Kusini

Mamlaka ya Sudan Kusini imesema kuwa takribani watu 81 wameuawa, wamekiwemo raia 26 wakati wa mapigano kati ya raia wenye silaha na wanajeshi wakati wa zoezi la kurejesha silaha. Msemaji wa jeshi amesema askari 30 ndio wamefariki na wengine wamejeruiwa.


Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kuwa watu wapatao 130 wameuawa.


Serikali ilikuwa inafanya zoezi la kuchukua silaha ambazo zinamilikiwa na raia baada ya rais Salva Kiir kutangaza mwezi Julai kuwa zoezi hilo lifanyike ili kusaidia kumaliza vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa kuziondoa silaha kwa raia.


Inadhaniwa kuwa kuna mamilioni ya bunduki zinazomilikiwa na raia.


Lakini baadhi ya raia ambao ni jamii ya wafugaji , wanataka serikali kuwahakikisha usalama wao kabla hawajakabidhi bunduki zao.




Post a Comment

0 Comments