Loading...

Aug 12, 2020

Huu hapa ujumbe wa morrison kwa mashabiki zake

 KIUNGO wa Yanga Bernard Morrison ametuma ujumbe kwa mashabiki wake akiwataka washushe presha kwa sasa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Morrison ametupia video akionekana akichezeza mpira na kuweka ujumbe uliosema kuwa:" Tulieni msiwe na presha,"Kwa sasa Morrison yupo kwenye mvutano mkubwa na Yanga kuhusu suala lake la mkataba ambapo shauri hilo limeanza kusikilizwa Agosti 10 na 11. Siku zote mbili hakuna majibu ambayo yalitolewa zaidi ya maelezo kuwa bado shauri linaskilizwa.


Leo Agosti 12 linatarajiwa kuskilizwa tena na hukumu inatarajiwa kutolewa leo na Kamati ya Hadhi ya Wachezaji ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF).


Shauri hilo pia lina mvutano mkubwa baada ya Simba kumtangaza mchezaji huyo Agosti 8 kuwa mali yao ilihali alikuwa ana kesi haijatolewa hukumu.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger