Waziri wa mambo ya nje wa Lebanon ajiuzulu

Waziri wa Mambo ya nje wa Lebanon Nassif Hitti amewasilisha barua ya kujiuzulu kwake kwa Waziri Mkuu Hassan Diyab.

Afisa wa serikali, ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema kwamba Waziri wa Mambo ya nje Hitti aliwasilisha barua ya kujiuzulu kwake kwa Waziri Mkuu Diyab.

Kwa mujibu wa habari waziri huyo amesema kwamba kujiuzulu kwake ni hatua ya mwisho isiyoweza kubadilishwa.

Hitti bado hajatoa taarifa kuhusu sababu ya kujiuzulu.

Post a Comment

0 Comments