Na Faruku Ngonyani, Mtwara.
Leo tarehe 30 Septemba 2020 Mzee Mohamedi Natosa amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mtwara Vijijini.
Uundwaji wa Baraza hilo la Wazee kutarahisisha kusikiliza na kutatua changamoto walizonazo wazee hao.
Viongozi wengine waliochaguli ni Pamoja na Amina Mnikosa (Makamu Mwenyekiti), Mohamedi Mkolamambo (katibu), Manfred Sankwa (Katibu Msaidizi), Hadija Mninde (Mwekahazina) na Zainabu Ngumbo (Mwekahazina Msaidizi).
Kiapo Cha Uadilifu kwa Viongozi wa Baraza hilo la wazee limesimamiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya katika Ukumbi wa mikutano Sabodo Sekondari.
Mkuu huyo wa Wialya amesema kuwa Sheria ya Wizara ya Afya ya Mwaka 2003 inatambua uwepo wa Mabaraza ya Wazee Kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata na Halmashauri kwa minajili ya kuweza kuwafikia na kuwapa huduma stahiki za kijamii.
Amewataka wazee kuwatumia Viongozi wao kwa namna ambayo itakuwa daraja la kutatua changamoto zao kiafya na Mambo mengine.
Pia amesisitiza uwajibikaji kwa wataalamu wanaosimamia stahili za wazee hao hasa Mganga Mkuu Wilaya, Afisa ustawi na Mratibu wa Mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa ngazi ya Jamii (CHF) kutoa huduama bila kuwakwaza.
