Botswana yawaruhusu wanawake walioolewa kumiliki ardhi


Mokgweetsi Masisi, pia amesema wajane na yatiba wataweza pia kumiliki ardhi ya kuishiImage caption: Mokgweetsi Masisi, pia amesema wajane na yatiba wataweza pia kumiliki ardhi ya kuishi

Wanawake walioolewa kwa mara ya kwanza wanaweza kumiliki ardhi pamoja na waume zao, amesema rais wa wanchi hiyo Mokgweetsi Masisi.

Hadi sasa, sera ya ardhi ya nchi hiyo inawazuwia wake kumiliki ardhi, kama wame zao tayari wana ardhi.

Ni wanawake ambao bado hawajaolewa ambao hawana ardhi ndio wanaokubaliwa kisheria kumiliki ardhi.

Ubaguzi huo uliwaasha mamilioni ya wanawakebila uwezo wa kupata ardhi katika maeneo wanamoishi na kufanya kazi.

Rais alitweet kwamba sheria iliyofanyiwa mabadiliko : "Kila Mbotwana atakuwa na uwezo wa kupata ardhi ya makazi katka eneo analochagua katika nchi, katika ardhi ya taifa nay a kikabila ."

Amesema kuwa sera mpya pia itawalinda wanane na yatima wanaoongoza familia na wanaohitaji ardhi kwa ajili ya makazi.

Makundi ya kutetea haki za binadamu wameafiki mabadiliko hayo wakisema yamechukua muda mrefu kufikiwa.



Post a Comment

0 Comments