Ifahamu historia ya mwigizaji Salman Khan

 

Desemba 27, 1965 alizaliwa mwigizaji wa filamu wa India, prodyuza na mwimbaji Salman Khan.

Jina lake halisi ni Abdul Rashid Salim Salman Khan. Nyota huyo alizaliwa katika mji wa Indore huko Madhya Pradesh nchini India.

Kwa asili ukoo wa Salman Khan umetokea Afghanistan. Vyanzo mbalimbali vinasema mababu wa Salman Khan (Alakozai Pashtuns) waliingia Indore miaka ya katikati ya 1800 wakitokea katika ardhi ya Kiafghan.

Salman Khan alizaliwa kwa wazazi  Salim Khan na mama Sushila Charak.

Salman Khan alianza kuwika tangu mwaka 1988 hadi sasa akionekana katika filamu mbalimbalimbali ikiwamo Biwi Ho To Aisi. Ana marafiki wengi kama Familia ya Sooraj Barjatya, Aamir Khan, Ajay Devgn, Sanjay Dutt, Anil Kapoor, Shahrukh Khan, Kabir Khan, Mini Mathur and David Dhawan. Watu wake wengine wa karibu ni Govinda, Rani Mukerji, Jackie Shroff, Prabhu Deva, Karisma Kapoor, Mithun Chakraborty, Farah Khan, Sajid-Wajid, Himesh Reshammiya, Akshay Kumar, Saif Ali Khan, Kareena Kapoor Khan, Katrina Kaif, Bhushan Kumar, Dharmendra, Sunny Deol, Bobby Deol, Shatrughan Sinha and family, na Sushmita Sen.

Salman Khan amekuwa katika medani ya filamu kwa miaka 30 akitwaa tuzo mbalimbali zikiwamo mbili za kitaifa.

Salman Khan amekuwa akichukuliwa na vyombo vya habari kuwa ni miongoni mwa wasanii wa filamu waliopata mafanikio makubwa katika medani hiyo nchini India na Kimataifa.

Mnamo mwaka 2018 Jarida la Forbes lilimtaja Salman Khan katika orodha ya wasanii 100 wenye kiasi kikubwa cha fedha kutokana na kazi yao.

Salman Khan alishika nafasi ya 82 kwa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 37.7 sawa na shilingi bilioni 86.4
Anafahamika sana nchini India kwa kuwa mtangazaji wa kipindi cha Televisheni cha Bigg Boss tangu mwaka 2010. Mnamo mwaka 1989 alitoka filamu nyingine Maine Pyar Kiya. 

Na kuanzia miaka ya 1990 hadi sasa ametoa filamu nyingi.  Mnamo mwaka 1993 Salman Khana alipata fursa ya kuigiza Baazigar na Abbas Mustan  lakini alikataa fursa hiyo na ndipo nafasi hiyo akapewa Shah Rukh Khan.

Mwaka 1999 alikumbwa na kesi akiwa mwigizaji mwenzake Hum Saath Saath Hain wakistakiwa kwa kosa la kumuua swala mweusi na chinkara wakati wakishuti filamu  kule Jodhpur, Rajasthan.

Aprili 5, 2018 alipatikana na kosa na alihukumiwa  miaka mitano na mahakama ya Jodhpur.

Hakimu Dev Kumar Khatri alisema Salman Khan amehukumiwa kwa kifungu cha sheria Na. 51 cha Uhifadhi wa Wanyamapori. Hata hivyo alitolewa kwa dhamana baada ya kushinda siku mbili katika jela ya Jodhpur.

Mnamo mwa 2002 alikutwa na kesi ya kugonga na kukimbia. Katika tukio hilo Salman Khan alikuwa akiendesha gari kwa mwendo kasi ambapo liliacha njia na kwenda kulivaa jengo la kutengeneza mikate  na kumuua mtu mmoja na wengine watatu kujeruhiwa  kwenye ajali hiyo.

Watu hao walikuwa wamelala kwenye kibaraza cha jengo hilo. Salman Khan amekuwa mtu wa matukio kwani mwaka 2008 alipigana na Shah Rukh Khan katika sherehe ya kuzaliwa kwa Katrina Kaif.

Pia Desemba 2017 Salman Khan na msanii wenzake Shilpa Shetty walikamatwa na Polisi ya Andheri, Mumbai kwa kitendo cha kutumia neno ‘Bhangi’ katika hadhira.

Post a Comment

0 Comments