Kembaki atembelea soko la Serengeti kuomba kura


Na Timothy Itembe Mara.

Mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi (CCM),Michael Kembaki jana ameamua kusaka kura kwa wajasiliamali wa soko la jioni maarufu Serengeti na kupokea kero.

Katika matembezi hayo,Kembaki aliamua kuwaomba kura wajasilia mali wadogo wakiwemo wafanyabiashara wa vibanda,wauzanyanya,wauza samaki,wamachinga,wauza mbogamboga na wengine ambapo aliwataka kuchagua ili aende kuwatumikia.

Mgombea huyo alisema kuwa akifanikiwa na kuwa mbunge atahakikisha anatatua kero zinazowakabili watu wa Tarime na wafanyabiashara wa soko la jioni la Serengeti.

Kembaki alitumia nafasi hiyo kutupia lawama mbunge aliyekuwepo wa upinzani anaye ende kumaliza mda wake kuwa alichaguliwa ili kuwaletea maendeleo wananchi lakini cha ajabu hakuwaletea maendeleo wananchi wake.

Kwa upande wa wauza mboga na wafanyabiashara wa soko la jioni la Serengeti walimuomba Kembaki kuwasemea bungeni matatizo ambayo yanawakabili  ikiwemo kodi mbalimbali ambazo nikero katika soko hilo la jioni Serengeti.

“Mgombea umefanya kitu cha maana kututembelea ili kujua shida zetu ndani ya soko letu tulipo tunasumbuliwa na watu wa Tanroad kuwa maeneo tunayofanyia biashara ni yakwao tunaomba tuandaliwe maeneo mengine bora ya kufanyia biashara badala ya kuendelea kusumbuliwa kila siku sasa tunaomba sisi wamiliki wa meza za matunda na wafanyabiashara wengine eneo hili tusisumbuliwe katika biashara zetu”alisema Anastazia Nyanga.

Mjasilia mali huyo aliongeza kusema kuwa eneo hilo wanalipia shilingi 25,000-30,000 kwa mwezi wanalipa fedha ya  mlinzi shilingi 5,000 kwa mwezi,ambapo kodi zote zikiunganishwa hawapati faida fedha yote inaishia kwenye kodi na wengine tunategemea biashara hiyo kulipa mikopo.

Naye Pendo Elias aliomba kuboreshewa soko la kufanyia biashara na kuachana na soko la Serengeti ambapo wanakimbizana na wana mgambo wa halmashauri pia wakibugudhiwa katika eneo hilo na wanapata  hasara ambazo hazitarajiwi kwenye biashara wanazofanya.

Elias aliongeza kuwa wakichelewa kulipa kodi hizo wanajikuta  mabanda yao ya biashara yakisukumwa  mbali hata kama kuna mali ndani yake,kwa hali hiyo tunaomba ukifanikiwa na kuwa mbunge ututetee ili tuwe tunafanyabiashara zetu kwa uhuru.

Post a Comment

0 Comments