Kiongozi wa Catalonia kuondolewa madarakani na Uhispania

 


Mahakama kuu ya uhipania imetowa uamuzi leo unaosema kwamba kiongozi wa jimbo linalotaka kujitenga la Catalonia Qium Torra ataondolewa madarakani kwa utovu wa nidhamu . 

Mahakama hiyo kwa sauti moja imethibitisha uamuzi uliotolewa na mahakama ya jimbo hilo la Catalonia mwaka jana ambao Torra aliukatia rufaa. 

Uamuzi huo ulitowa amri kwamba Torra mwenye umri wa miaka 57 hawezi kuendelea kubakia kwenye ofisi ya umma kwa miezi 18. 

Kadhalika kiongozi huyo wa jimbo la Catalonia anatakiwa kulipa faini ya yuro 30,000 na kukabidhi nafasi yake kama waziri mkuu wa jimbo hilo kwa naibu wake Pierre Aragones.

Ripoti za vyombo vya habari zinaeleza kwamba hatua hiyo itachukuliwa wiki hii. Hatua hiyo inamaanisha Aragones atatarajiwa kuitisha uchaguzi mpya mwanzoni mwa 2021. 

Kosa la Torra ni kukataa kuondowa nembo na mabango ya vuguvugu la kudai uhuru wa Catalonia katika ofisi yake na majengo ya umma kabla ya uchaguzi wa mwaka uliopita, kama alivyotakiwa na tume ya uchaguzi.


Post a Comment

0 Comments