Kuchelewa kusambazwa vifungashio, Ma DC wanena

 


Na Ahmad Mmow, Lindi.

Kuchelewa kusambazwa vifungashio  katika vyama vya msingi vya ushirika( AMCOS)

kutoka kwa vyama vikuu vya ushirika vya Lindi Mwambao na RUNALI kumetajwa kunaweza kusababisha wakulima wa korosho kuuza nje ya mfumo rasmi( kangomba).

Hofu hiyo imebainishwa na mkuu wa wilaya ya Lindi na Kilwa walipozungumza wakati wa mkutano wa wadau wa korosho, ufuta na mbaazi mkoa wa Lindi uliofanyika jana mjini Lindi.

Shaibu Ndemanga ambaye ni mkuu wa wilaya ya Lindi alisema ucheleweshaji vifungashio unaosababisha changamoto ya uhaba wa vifungashio kwakiasi fulani unachangia wakulima wa korosho kuuza zao hilo nje ya mfumo rasmi( kangomba) na malalamiko kutoka kwa wakulima.

" Korosho zipo ndani majumbani, minada bado lakini wakulima wanaombwa wasiuze kwakangomba. Sasa tunavurugana huko," alisema Membe.

Ndemanga alisema kwamsimu huu wa 2020/2021 tayari zoezi la vifungashio limeshindwa kufanyika kwa wakati. Hali inayoweza kusababisha korosho kuchelewa kununuliwa. 

 Alisema nijambo la kushangaza kusikia vyama vikuu vimeingia mikataba nakampuni zinazo uza magunia nakuweka tarehe isiyokubalika na haipo kuwa nitarehe ya mwisho ya kampuni hizo kupeleka vifungashio kwa vyama vikuu hivyo.

" Kama Union imeingia mkataba na  kwamba kampuni zipeleke vifungashio siyo zaidi ya tarehe 31.09.2020 tarehe ambayo haipo kwenye kalenda inashangaza sana. Mwezi Septemba hauna siku 31. Lakini wanasema mwisho tarehe 31, kama kampuni isipotekeleza wataibanaje?," alisema na kushangaa Ndemanga.

Mashaka ya Ndemanga yaliungwa mkono na mkuu wa wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai ambaye alisema kuchelewa kusambazwa vifungashio kunasababisha malalamiko toka kwa wakulima ambao tayari wamevuna korosho. Akitolea mfano kata ya Pande wilaya ya Kilwa ambako wakulima tayari wamevuna korosho na zipo majumbani.

Mashaka ya wakuu hao ya wilaya yaliungwa mkono na mhasibu mkuu wa chama cha msingi cha ushirika(AMCOS) Nambambo, Hanafi Mwita ambaye alisema kuchelewa kusambazwa vifungashio kunachangia wahasibu wakuu wa AMCOS kushindwa kubaini haraka ubadhirifu unaofanywa na baadhi ya viongozi na watendaji wasio waadilifu wa matawi ya AMCO.

Alisema uhaba wa vifungashio unasababisha wahasibu wakuu kushindwa kufunga hesabu kwani korosho zinarundikana maghalani. Kwahiyo wanajikuta wanashindwa kubaini wizi na kuchukua hatua zinazostahili kwawakati.

Post a Comment

0 Comments