Maandamano dhidi ya serikali yawajerui wengi Cameroon

 

Raia mmoja ameuawa na wengine kujeruiwa nchini Cameroon katika maandamano ya kuipinga serikali kufanyika maeneo mbalimbali nchini humo siku ya Jumanne, kwa mujibu wa wakili wa chama cha upinzani.

Wakili huyo, bwana Robert Amsterdam, ameweka kwenye kurasa ya tweeter video ya mwandamanaji akiwa amelala na hapumui.

Aliandika: "Tumepokea ripoti kuwa muandamanaji mmoja alipigwa risasi na kuuawa na polisi katika mji wa Douala na wengine wengi walikuwa wamejeruhiwa na kukamatwa."

Serikali ilitoa onyo dhidi ya maandamano hayo yaliyohamasishwa na kiongozi wa upinzani Maurice Kamto.

Waandamanaji walitaka mgogoro wa 'Anglophone' ufikie tamati na mabadiliko yawekwe kwenye utaratibu wa uchaguzi.

Bwana Kamto amesema kuwa kama masuala mawili aliyopendekeza hayatafanyiwa kazi , basi maandamano yataendelea mpaka rais Paul Biya atalazimka kutoka madarakani.

Bwana Biya amekuwa madarakani tangu mwaka 1982. Alichaguliwa tena mwaka 2018 katika uchaguzi ambao bwana Kamto aidai kuwa ameshinda.



Post a Comment

0 Comments