Makamu wa Rais atangaza neema kwa wakulima wa Mahindi wilayani Ludewa

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Serikali imetangaza kuanzishwa kwa kituo cha kununua mazao ya mahindi wilayani Ludewa mkoani Njombe,kutokana na changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakumba wakulima wa zao hilo pindi wanapohitaji kuuza mazao yao.


Makama wa Rais ambaye pia ni mgombea mwenza wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mpainduzi.Akizungumza na wananchi wa Mlangali kwenye mkutano wa kuomba kura amesema kutokana na changamoto ya Soko ndani ya wilaya ya Ludewa amezungumza na wakala wa Taifa wahifadhi wa Chakula (NFRA) ambao wameahidi kuanzisha kituo cha kununua zao la mahindi wilayani humo.


“Nikiwa Ludewa nilisikia kuna changamoto ya soko kwenye mazao ya chakula,Niwape habari njema kuwa kuanzia wiki ijayo haitazidi Ijumaa NFRA watakuwa hapa wameanzisha kituo cha kununulia mahindi” alisema Samia Suluhu Hassan


Vile vile katika sekta ya elimu,mgombea mweza amezungumzia kuhusu ujenzi wa chuo cha ufundi (VETA) chama mkoa wa Njombe kinachojengwa wilayani Ludewa.


“Ndani ya wilaya hii ya Ludewa pale Shaurimoyo,serikali inajenga chuo cha ufundi Veta lakini kilisimama kwa muda kwasababu ya uzembe wa mkandarasi na sasa serikali imeingilia kati tumeondo mkandarasi mzembe”alisema Samia Suluhu Hassan Mgombea mwenza wa Urais JMT kupitia CCM


Aidha amesema “Tumeita tenda wakandarasi wengine wameomba na punde watarudi kumalizia chuo cha ufundi pale Shaurimoyo” aliongeza Samia Suluhu Hassan Mgombea mwenza wa Urais


Naye mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Ludewa Mh,Joseph Kamonga amewatia moyo wananchi wa Ludewa juu ya serikali kukamilisha ujenzi wa chuo cha ufundi huku akiishukuru serikali kuonyesha nia ya kukamilisha ujenzi


“Ludewa tumependelewa sana.Serikali imeonyesha nia ya kukamilisha Chuo cha VETA Shaurimoyo ili vijana watakaopewa ujuzi wa aina mbali mbali pale waweze kuajiliwa kwenye viwanda ikiwemo Mchuchuma na Liganga” alisema Joseph Kamonga


Baadhi ya wananchi wa Mlangali wanasema kujengwa kwa chuo cha ufundi kwenye wilaya yao kutasadia kwa kiasi kikubwa wananchi kupata ujuzi mbali mbali utakao wawezesha kupata ujuzi.

Post a Comment

0 Comments