Loading...

Sep 15, 2020

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yataka Ulaya kuchukua wakimbizi zaidi kutoka Ugiriki

 


Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema leo kuwa mataifa ya Ulaya yanahitaji kuwachukua wahamiaji zaidi kutoka Lesbos pamoja na makambi mengine yaliyojaa watu katika visiwa vingine vya Ugiriki. 

Mkuu wa shirika la kimataifa la kuwahudumia wahamiaji IOM Antonio Vitorino amesema katika taarifa kuwa inahitajika nia thabiti ya kuwachukua wakimbizi katika nyakati hizi ngumu wakati Umoja wa Ulaya unatayarisha mfumo ambao unaweza kufanya kazi chini ya wajibu wa kugawana majukumu. 

Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR nchini Ugiriki Philippe Leclerc, amesema kuwa idadi ya watu katika vituo vya kuwahifadhia wakimbizi katika visiwa vya Ugiriki wanapaswa kupunguzwa na mazingira ya kuishi ni lazima yawe bora.


KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger