Loading...

Sep 21, 2020

Mgombea mwenza CHADEMA apata ajali

 


Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama  Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu amepata ajali eneo la Msoka Kata ya Ngogwa, Jimbo la Masalala mkoani Shinyanga, wakati wakitoka  kwenye mkutano wa Kampeni katika jimbo hilo.


Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Afisa Habari wa CHADEMA Tumaini Makene  kupitia ukurasa wake wa twitter leo Septemba 21 amesema kuwa gari alilokuwa anatumia Mgombea Mwenza wa Urais CHADEMA amepata ajali na wote waliokuwa kwenye gari hiyo ni wazima wa afya.


“Tunamshukuru Mungu kwa kuwaponya katika ajali hii mbaya wote waliokuwa kwenye gari hii inayotumiwa na mgombea wa kiti cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Salum Mwalimu Juma Mwalimu” ameandika Tumaini Makene.


Aidha Makene amesema kuwa mgombea mwenza huyo anaendelea vizuri na amefanikiwa kukamilisha mkutano wake Kahama.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger