Mgombea udiwani aahidi ujenzi wa nyumba za watumishi

 


 Na Hamisi Nasri, Masasi

  Mgombea udiwani kata ya Lulindi jimbo la Lulindi Halmashauri ya wilaya ya Masasi, mkoanj Mtwara, kwa chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Dadi Musa ameahidi kujenga nyumba za watumishi katika shule ya msingi na ofisi zingine za seriakli ambazo zinachangamoto ya upungufu wa nyumba za watumishi.

  Aliyasema hayo jana wilayani Masasi alipokuwa akuomba kura kwa wananchi wa kata hiyo ya Lulindi kupitia mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Lulindi, kata ya Lulindi wilauani Masasi.

  Musa alisema iwapo akichaguliwa kuwa diwani kata ya Lulindi atahakikisha anatatua changamoto ya ukosefu wa nyumba za watumishi katika ofisi za serikali zilizopo katika kata hiyo, ikiwemo shule ya msingi Lulindi sasa.

  Alisema kitu kikubwa kilichomsukuma kugombea kiti cha udiwani katika ya Lulindi ni uwepo wa changamoto lukuki zilizopo na kila diwani anayechaguliwa hakuna maendeleo anayoyafanya ndani ya kata hiyo.

  Musa alisema ukosefu wa nyumba za watumishi kwenye ofisi mbalimbali zilizopo katika kata hiyo zinawapunguzia ufasi wa kufanya kazi watumishi hivyo kuzorotesha upatikanaji wa maendeleo kwa haraka.

  "Iwapo mkinichagua kuwa diwani wenu nitajenga nyumba za watumishi ndani ya kata hii ili kupunguza tatizo la ukosefu wa nyumba za watumishi na nitaanza kujenga nyumba za walimu katika shule ya msingi Lulindi naomba mniamini," alisema Musa

   Alisema changamoto zingine ambazo atashughulika nazo ni pamoja na ukosefu wa maji safi na salama ambapo atahakikisha mifumo ya maji iliyokufa anaifufua na huduma hiyo inarejea kama wakaida.

  Musa alisema kata ya Lulindi inakabiliwa na tatizo la miundombinu ya barabara hivyo iwapo akichaguliwa kuwa diwani barabara hizo zitatengenezwa chini ya usimamizi wake.

  Kwa upande wake mwenyekiti wa Chadema jimbo la Masasi mara baada ya kumnadi mgombea huyo alisema wananchi wasichaguwe viongozi kwa ushabiki wa vyama.

   Alisema wanapaswa kuchagua kwa kuangalia sera bora zinazotolewa na mgombea na uwezo mgombea huyo kuleta maendeleo kwenye maeneo yao.

Post a Comment

0 Comments