Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo amefufua malumbano na makao makuu ya kanisa Katoliki leo wakati wa ziara yake mjini Rome, mwezi mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa Marekani na akiwa katika mbio za kidiplomasia ambazo wataalamu wanaziona kama juhudi za kuwavutia wapiga kura wahafidhina katika kanisa katoliki.
Wachambuzi wanasema kuwa papa amekasirishwa na miito ya wazi ya Pompeo kutaka kutupiliwa mbali makubaliano ya kihistoria kati ya China na Vatican.
Chanzo katika kanisa Katoliki kimesema, Pompeo hatakutana na kiongozi wa kanisa hilo papa Francis kwasababu kiongozi huyo wa kidini anaepuka mikutano kama hiyo katika kipindi hiki cha uchaguzi.
