Tanzania yaruhusu ndege za Kenya kutua


Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), imeruhusu ndege zote zinazotoka Kenya kuanza kutua nchini humo baada ya kuondolewa vikwazo vilivyokuwa vimewekwa.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari imeeleza kuwa mbali na KQ, zuio hilo limeondolewa pia kwa Fly 540 Limited, Safarilink Aviation  na AirKenya Express Limited.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja tangu Kenya ilipoijumuisha Tanzania katika orodha ya nchi 147 ambazo raia wake au wageni kutoka katika nchi hizo hawatotakiwa kukaa karantini kwa siku 14 kuthibitisha kuwa hawanamaambukizi ya virusi vya corona (COVID19).

TCAA imesema kuondolewa kwa zuio hilo kunaanza mara moja na tayari Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Kenya imejulishwa.

Post a Comment

0 Comments