Tetesi za soka kimataifa


 Barcelona imewasiliana na Arsenal kuhusu uhamisho wa beki wa kulia Mhispania Hector Bellerin, 25. (Sport - in Spanish)

Mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain pia wanamtaka Bellerin na imeshawasiliana na wawakilishi wake. (Independent)

Real Madrid wako tayari kulipa nusu ya mshahara wa mwaka wa Gareth Bale ili kusaidia mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 raia wa Wales kuondoka katika timu hiyo ya Hispania. (Telegraph - subscription required)

Mshambuliaji wa Everton na Italia Moise Kean, 20, anataka kurudi Juventus, klabu aliyotoka kabla ya kijuiunga na Toffees mwaka 2019. (Calciomercato - in Italian)

Rennes imethibitisha kuwa wako kwenye mazungumzo na Chelsea kwa ajili ya Kipa Msenegali, Edouard Mendy, 28. (Goal)

Meneja wa England Gareth Southgate atafanya mazungumzo na kiungo wa Manchester City Phil Foden, 20, na mshambuliaji wa Manchester United Mason Greenwood, 18, baada ya nyota hao kuvunja masharti ya corona wakiwa na timu ya taifa. (Mail)

Bournemouth wanataka kumsainisha kiungo wa pembeni wa Scotland na Newcastle Matt Richie lakini wamekwama kukubaliana na masharti binafsi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Newcastle Chronicle)

Mlinzi wa kati wa Arsenal na Brazil David Luiz, 33, huenda akaukosa mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa msimu huu kufuatia majeraha ya shingo. (Telegraph )

Aston Villa inataka kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na Norway Joshua King, lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 28-anapendelea zaidi kutua Manchester United baada ya uhamisho wake kwenda Old Trafford kukwama kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi January. (Athletic - subscription required)

Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 29, atatafuta ufafanuzi zaidi kuhusu majukumu yake kwenye timu wakati huu tetesi zikisema washika bunduki hao wanataka kumuuza msimu huu. (ESPN)

Aston Villa imeongeza dau zaidi linalovuka £15m kwa ajili ya kumnasa Kipa wa Arsenal Muargentina Emiliano Martinez, 28, baada ya dau lake la kwanza kugonga mwamba. (Goal)

Watford haitamzuia mshambuliaji wake raia wa England Troy Deeney, 32, kutaka kurejea kukipiga Ligi kuu nchini Uingereza. (Mail)

Manchester United imekamilisha usajili wa mshambuliaji Alejandro Garnacho,16, kutoka Atletico Madrid. Kinda huyo atawasili kutoka Hipsania baadae wiki hii, na atapaswa kukaa karantini kwa siku 14 days. (Manchester Evening News)

Nottingham Forest wanajiandaa kukamilisha usajili wa beki wa Paris St-Germain na timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 21 ya Ufaransa, Loic Mbe Soh, 19. (Goal - in French)

Kiungo wa pembeni wa QPR Bright Osayi-Samuel, 22, anataka Crystal Palace iweke ofa ili kumnasa. (Sky Sports)

Post a Comment

0 Comments