Uturuki, Ugiriki zaridhia mazungumzo kutanzua mzozo baina yao.

 


Uturuki na Ugiriki zimekubaliana kuanza mazungumzo yenye lengo la kumaliza mzozo wa utafutaji wa gezi katika eneo linalogombaniwa la mashariki mwa bahari ya Mediterania na Aegean. 

Hayo yametangazwa na Ikulu ya Uturuki mjini Ankara, baada ya mazungumzo kati ya viongozi wa Uturuki, Ujerumani na Umoja wa Ulaya. 

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel wamefanya mkutano kwa njia ya video, na kuafikiana kuwa msukumo uliopo kutokana na mchakato wa mawasiliano unapaswa kuendelezwa na pande hizo mbili. 

Rais Erdogan ameelezea matumaini yake kuwa katika mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya utakaofanyika Alhamis na Ijumaa mjini Brussels utaleta ari mpya ya uhusiano mwema baina ya Umoja wa Ulaya na Uturuki.


Post a Comment

0 Comments