ZANZIBAR: Naibu katibu Mkuu CCM kufanya kampeni za kisayansi

 


Na Thabit Madai,Zanzibar.

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Dk. Abdullah Juma Saddala (Mabodi) amesema kwamba Chama cha Mpinduzi CCM mwaka huu Kimeamua kufanya kampeni za kisayansi ambapo kila mwanachama wa chama hicho anayo fursa ya kunadi Sera pamoja na kuwanadi wagombea wa chama hicho.


Hayo ameyaeleza leo katika Mkutano Mkuu wa hadhara wa kumnadi Mgombea wa Urais wa Zanzibar DK. Hussein Mwinyi pamoja na wagombea w nafai mbalimbali kupitia chama hicho cha Mapinduzi ya Zanzibar, Mkutano huo wa Hadhara umefanyika katika kiwanja cha Shule ya Nungwi alimaarufu kiwanja cha Mapara,Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.


Dk.Mabodi amesema kwamba Kamati kuu ya chama hicho kimeaa na kupitisha kuwa kampeni za mwaka huu ziwe za kisayansi ambapo kila mwanancham wa chama hicho awe na fursa sawa ya kunadi sera pamoja na kuwanadi wagombea wa chama hicho.


Alisema kwamba tayari Mgombea wa Urais wa Zanzibar ameshaanza kkutekeleza kwa vitendo maagizo ya kamati kuu kwa kufanya kampeni ambazo zitawashirikisha moja kwa moja wananchi katika maeneo husika.


“Dk. Mwinyi ameshakutana na Wananchi wakiwemo wavuvi,wakulima pamoja na wananchi kwa ngazi ya chini kabisa kwa lengo la kunadi sera za chama cha Mapinduzi CCM,”Alisema Dk. Mabodi


 Katika hatua nyingine Dk. Mabodi akiichambua ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020/2025 alisema, ni ilani ambayo inatekelezeka kwa vitendo utokana inazingatia maslahi mapana ya umma kwa wananchi wake.


Alisema, Ilani hiyo imesema itaendeleza jitiihada za kuunganisha wazanzibar wote na kuwa wamoja lakini pili kuhakikisha maendeleo ya uchumi yanazngatia usawa na yananufaiha maeneo yote ya Zanzibar kwa maana ya Unguja na Pemba.


Lakini pia alisema,  ilani ya chama cha Mapinduzi pia itaendelea kuwanafaisha wananchi wa nafasi zote pamoja na kuimarisha upatikanaji wa ajira kwa vijana.


"Hii ni ahadi kwa vijana kwani katika ilani yetu iliyopita karibu vijana laki tatu wamepata ajira katika awamu ya saba sasa na awamu ya nane ya Dk Mwinyi ina neema tele," alisema.


Lakini pia alisema, jambo jengine ambalo lipo katika ilani hiyo ni kupitia upya mfumo wa elimu wa ufundi wa amali ili vijana wengi waweze kupata ajira.


Aidha alisema, jambo jengine ni kuibua na kueneleza sekta mpya ya uchumi ambao ni uchumi wenye ubunifu, uchumi unaotekelezeka na uchumi wa kidigitali.


"Jambo jengine ni kuendeleza kilimo cha kisasa mambo mbayo tayari yameshaanza kutekelezwa na awamu hii, hivyo Dk Mwinyi kazi yake kubwa ni kuendeleza, kilimo chenye tija na kilimo kkilichotufanya sisi tuuze mazao yetu," alisema


Alisema, kuhusu kudumisha amani na utulivu hawana shaka na Dk Husseiin Ali Mwinyi kwa sababu yeye alikuwa Waziri wa Ulinzi hivyo anajua jinsi ya kuilinda amani iliyopo.


Alieleza kuwa chama cha Mapinduz kitapita katika kila mkoa na wilaya, kukutana na wananchii ili kuelezea mazuri yote yaliyofanywa na chama cha Mapinduzi ili wananchi wakiridhie chama hicho kiweze kuongoza tena nchi.


"Tumesikia mengi yamesemwa na kuna watu wanatishia amani, wanatutishia sisi nyau, lakini sisi tumesema tutahubiri amani, utulivu, mshikamano na maendeleo sasa kama kuna watu wanaona amani haina maana na wanajaribu kushawishi makundi ya watu kuivuruga, tunawaambia wazi kuwa hatutakubali kuvunjiwa amani," alisema


Lakini pia alichukua nafasi hiyo kuwaombea kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Johm Pombe Magufuli, Mgombea mwenza Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa ZZanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi, Wabunge, Wawaklishi na Madiwani wote wa CCM.

Post a Comment

0 Comments