Bado ulaji wa vyakula mbali mbali kitaifa ni tatizo- Waziri Hasunga


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Waziri wa kilimo nchini Tanzania Japhet Hasunga,ametoa witoa kwa watanzania kuongeza ulaji wa vyakula mbali mbali kwani umekuwa ni wa kiwango cha chini ukilinganisha na kiwango cha kimataifa wakati taifa limekuwa na uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula.

Waziri Hasunga ametoa wito huo mkoani Njombe wakati akifunga maonesho ya chakula yaliyofanyika kwa siku sita mkoani humo katika maeneo ya Mji Mwema yenye lengo la kutoa elimu ya chakula kuelekea kilele cha siku ya Chakula Duniani yaliyohitimishwa kitaifa mkoani Njombe

"Kitaifa ulaji wa vyakula mbali mbali ni asilimia 35.1% wakati mkoa wa Njombe na 23.9% hii inaashilia kuwa kwa pande zote mbili kitaifa na kimkoa,ulaji wa vyakula mbali mbali bado ni tatizo kwani ni chini ya 50% ya kiwango kinachokubalika kimataifa"alisema Japhet 

Amesema baadhi ya mikoa nchini ukiwemo mkoa wa Ruvuma yenye kiwango kikubwa cha uzalishaji bado imekuwa ikiongoza katika udumavu.

"Mkoa wa Ruvuma unaongoza kwa uzalishaji wa chakula lakini udumavu wa 41.0% wakati uzalishaji wa chakula hapa nchini kwa mkoa wa Ruvuma ni tani Milioni 1,251,511 na kiwango cha utoshelevu ni 237%"alisema Japhet Hasunga 

"Mikoa mingi ambayo inaongoza kwa uzalishaji wa chakula nchini,ulaji wao sio mzuri na wengi ndio wana udumavu mkubwa ukilinganisha na uzalishaji,kuna kila sababu ya kutoa elimu ya kutosha ili wale wanao zalisha zaidi waweze kula vizuri"Japhet Hasunga waziri wa kilimo

Vile vile ameitaja mikoa yenye kiwango kidogo cha udumavu "Mikoa yenye viwango vya chini zaidi ya udumavu ni Kilimanjaro yenye udumavu wa 20.0%,Dar es Salaam 20.1% , Mjini Magharibi 20.4% na mkoa wa kusini Pemba ni 20.8% hii ndio mikoa inayofanya vizuri upande wa udumavu"Japhet Hasunga  

Aidha amezungumzia hali ya ukondefu"Takwimu zinaonyesha udumavu umepungua kutoka 42% ya  mwaka 2010 hadi 32% mwaka 2018,Ukondefu umepungua kutoka 3.8% mwaka 2014 hadi 3.5 mwaka 2018 ambapo ni chini ya kiwango cha malengo ya mkutano wa afya duniaani cha 5%,Nchi tunafanya vizuri japo tunatakiwa tutokomeze kabisa"Japhet Hasunga waziri wa kilimo

Naye Zlatan Milsic Mwakilishi wa mashirika ya umoja wa mataifa Tanzania,amesema umoja wa mataifa utaendelea kushirikiana na Tanzani kutokomeza utapiamlo.

"Umoja wa mataifa utaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania,kuhakikisha tunatokomeza aina yote ya utapiamlo lakini vile vile kusaidia upatikanaji wa lishe bora kwa makundi maalum  ambao ni watoto chini ya miaka miwili  na akina mama wajawazito"alisema Zlatan Milsic

Ameongeza kuwa "Siku hii inahitimisha miaka 75 ya shirika la chakula na kilimo Duniani (FAO),tushirikiane sote kwa kuwapongeza kufikisha miaka 75 na kuwatakia heri kuendeleza shughuli za kupambana uhakika wa kilimo Tanzania"Zlatan Milsic 

Katarina Revocat ni katibu tawala mkoa wa Njombe amewashukuru washiriki wote katika maonesho hayo waliowezesha kuendelea kwa maonessho hayo huku akikiri kujifunza fursa nyingi juu uzalishaji wa chakula zilizopo mkoani Njombe.

Nao baadhi ya washiri wamesema maonesho hayo kufanyika mkoni Njombe imekuwa ni fursa kwa kuwa wamejifunza vya kutosha na maonesho hayo yatawasaidia katika uboreshaji wa lishe.


Post a Comment

0 Comments